Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Awataka Viongozi Kutekeleza Majukumu kwa Kufuata Sheria
Oct 27, 2017
Na Msemaji Mkuu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akila kiapo cha kushika wadhifa huo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Jonas Kamaleki - MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi walioapishwa kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria katika kuwatumikia wananchi.

Rais Magufuli amayasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha, Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa aliowateua jana.

Amewataka viongozi hao kuwatumikia wananchi kwa kuongeza ubunifu ili kuinua uchumi na kutatua kero zao hasa za wananchi wanyonge.

“Nataka mkawe sauti yao, mumtangulize Mungu katika kuwatumikia watu wake,”aliwaasa Rais Magufuli.

[caption id="attachment_21119" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaini hati ya kiapo cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi mara baada ya kula kiapo hicho leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Rais Magufuli amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa bidii ili kujenga Tanzania mpya yenye uchumi mzuri na kuifanya nchi kuwa ya kuvutia.

Aidha, Rais Magufuli amewaambia wakuu wa mikoa waangalie nini kinaweza kufanyika katika maeneo yao ili kuinua uchumi wa wananchi waishio katika mikoa hiyo.

Akizungumza kuhusu Makatibu na Manaibu wao, Rais Magufuli amewataka watatue kero na changamoto zilizopo kwenye wizara zao.

“Nyote niliowateua msijifanye wageni katika wizara au mikoa yenu, leo nikitaka kujua habari za korosho Ruvuma nakupigia simu na nataka nizipate hapo hapo,” alisema Rais Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi mara baada ya kumuapisha kushika wadhifa huo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa viongozi hao wameapa kuwatumikia wananchi bila upendeleo wala ubaguzi na kuwataka wafanye hivyo hivyo maana kiapo kinaduma.

“Wakuu wa mikoa tungependa kuona utumishi uliotukuka kutoka kwenu,” alisema Mhe. Samia Suluhu.

Amewataka Wakuu wa mikoa kuwa makini katika kufanya maamuzi na kuwaambia wafikiri mara tatu kabla ya kufanya maamuzi kwa kuangalia athari za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

[caption id="attachment_21121" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti akila kiapo cha kushika nafasi hiyo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Naye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai ameahidi kutoa ushirikiano kwa viongozi walioapishwa ili kuijenga Tanzania.

Akitoa salamu zake katika hafla hiyo, Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amesema viongozi walioapishwa wazingatie sheria katiak utekelezaji wa majukumu yao.

  [caption id="attachment_21122" align="aligncenter" width="750"] Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nicholaus Benjamin William akila kiapo cha kushika wadhifa huo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Amewataka wakuu wa mikoa kufanya kazi zao kwa uadilifu kwani wao ndio wenyeviti wa kamati za maadili za mikoa, hivyo hawapaswi kulalamika kuhusu uadilifu.

Rais Magufuli amewaapisha Makatibu Wakuu 4, Manaibu 7 na Wakuu wa Mikoa 6 ambapo Rais amembadilishia kituo cha kazi Mhe. Christina Mdeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma badala ya Dodoma na kumhamisha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge kwenda Dodoma.

  [caption id="attachment_21123" align="aligncenter" width="768"] Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nicholaus Benjamin William akisaini hati ya kiapo cha kushika wadhifa huo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_21124" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nicholaus Benjamin William mara baada ya kumuapisha kushika wadhifa huo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_21125" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi walipokutana katika hafla ya kuwaapisha Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu pamoja na Wakuu wa Mikoa leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_21126" align="aligncenter" width="1000"] Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu walioapishwa pamoja na Baadhi ya Mawaziri mara baada ya hafla ya kuwaapisha leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.(Picha na: Frank Shija )[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi