Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Apongezwa Kwa Kutia Chachu Mapambano Dhidi ya Malaria
Jun 27, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_4493" align="aligncenter" width="720"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikabidhi dawa za Viuadudu kwa baadhi ya wawakilishi wa Halmashauri nchini leo mjini Kibaha, Pwani. (Picha na WAMJW)[/caption]

Na: WAMJW, Kibaha

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,J nsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuongeza chachu katika mapambano dhidi ya malaria baada ya kwa kununua lita laki moja na kusambazwa kote nchini.

Ameyasema hayo wakati wa zoezi la ugawaji wa Viuadudu vya kutokomeza mazalia ya mbu wa malaria kwa halmashauri kumi na moja zilizofika katika kiwanda cha kuzalisha Viuadudu hivyo kilichpo Mjini Kibaha

“Namshukuru Mhe. Rais kwa kuruhusu kuanza zoezi hili la kugawa Viuadudu kwa awamu ambapo kwa awamu ya kwanza Viuadudu hivyo tunavigawa kwa Halmashuri 14 nchini ambazo zina viwango vikubwa vya maambukizi ya ugonjwa wa malaria,hii ametupa nguvu na ari sisi tuliopo kwenye dhamana ya kusimamia sekta ya afya katika kupambana na Malaria,”alisema Ummy Mwalimu

 

Akizungumzia kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo wa Malaria Waziri Ummy alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonyesha kwamba kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria nchini ni asilimia 14 ambapo katika kila watoto walio chini ya miaka mitano kati ya watoto 100 watoto 14 wamekutwa na maambukizi ya Malaria.

Aidha Waziri Ummy alitoa maelekezo kwa kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya ni kuhakikisha dawa hii inatumika kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Wizara ya Afya, ikiwemo kuangalia ukubwa wa eneo la mazalia ya mbu,na kiasi kinachotakiwa kupulizia.

Waziri Ummy amewataka wahakikishe wanapulizia Viuadudu hivyo angalau mara nne kwa mwezi kwa maana kila baada ya siku saba,hivyo ni lazima wanunue vifaa vya kupulizia dawa hii pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi watakaenda kufanya zoezi hilo.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy aliwaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuahkikisha ifikapo mwisho wa mwezi huu wawe wampelekee mahitaji halisi ya Viuadudu ili kuona ni jinsi gani watatekeleza zoezi hilo katika awamu zinazofuata.

 “Lazima nipate mahitaji halisi toka Halmashauri kwa kuwa Mhe. Rais ameshatuonyesha njia na ametuelekeza badala ya kununua dawa pia tununue na viuadudu hivi,” alisisitiza Waziri Ummy.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidi kutoka Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhandisi Elli Pallangyo alizitaja Halmashauri kumi na moja ambayo ni sawa na Mikoa sita zilizofika katika uzinduzi huo wa ugawaji wa Viuaduddu kwa awamu ya kwanza.

Halmashauri hizo pamoja na mgawo lita kwenye mabano ni Liwale (1,200), Tarime (384), Misungwi (1,296), Kasulu (540), Songea (816), Kakonko (660), Kisarawe (720), Kyerwa (1,080), Rufiji (5,088), Geita (2,100), Kilombero (1,140)

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi