Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Onorius John Njole kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria (Chief Parliamentary Draftsman – CPD).
Uteuzi wa Bw. Njole umeanza leo tarehe 23 Mei, 2019.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Njole alikuwa Mkurugenzi wa Sheria na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).
Bw. Njole anachukua nafasi ya Bi. Sara K. Barahomoka ambaye anastaafu.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Mei, 2019