Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Aipongeza Taasisi ya Mkapa, yakabidhi nyumba 50
Jul 10, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_6085" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita baada ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa kukabidhi nyumba 50 kwa wizara ya Afya.

[/caption] [caption id="attachment_6084" align="aligncenter" width="750"] Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita kabla ya kukabidhi Hati za umiliki wa nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa hiyo mitatu.[/caption]

(PICHA NA IKULU)

Na. Immaculate Makilika

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ameipongeza Taasisi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa kwa kukabidhi nyumba 50 Wilayani Chato kwa watumishi wa sekta ya afya na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo.

Akihutubia wananchi katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita, ambapo Taasisi ya Mkapa iliyojenga nyumba hizo kwa mikoa ya Geita, Kagera na Simiyu, Rais Magufuli alisema anashukuru Mfuko wa Dunia wa kupambana magonjwa ya Kifua Kikuu, UKIMWI na Malaria kwa kushirikiana na Taasisi ya Mkapa kwa kutoa pesa za ujenzi wa nyumba kwa ajili ya watumishi wa sekta ya afya katika mikoa 17 nchini.

“Nakushukuru sana Mzee Mkapa, hata baada ya kustaafu umeendelea kusaidia Watanzania, mnafanyakazi ya malaika ya uponyaji, ningeomba msichoke kuendelea kuwasaidia Watanzania”

Alisisitiza: “Taasisi zinazotuambia kuwa ni sawa watoto wa kike wakipata mimba wakiwa shuleni msizipe fedha badala yake mzipe taasisi kama hii ya Mkapa inayojenga majengo. Wasije hapa wakaaribu heshima na tamaduni za Tanzania zilizojengeka kwa muda mrefu”.

Pia, Rais Magufuli ameshukuru Serikali ya Japani kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo kujenga shule na ukarabati wa hospitali ya Chato mkoani Geita.

Mheshimiwa Rais alieleza kuwa Serikali yake itaendelea kufanya kazi kwa bidii ili  kuwateteta na kuwasaidia wananchi wanyonge ambapo tayari serikali imetoa  tozo zaidi ya  80 kwenye kilimo na tozo zaidi ya tano kwenye uvuvi, huku akiwasisitiza wananchi kufanya kazi kwa bidii ili  kujenga maisha yao.

[caption id="attachment_6083" align="aligncenter" width="750"] Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akimkabidhi Hati za Umiliki wa nyumba 50 za Watumishi wa Afya kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika uwanja wa michezo wa Mazaina Chato mkoani Geita.[/caption]

“Nina kuahidi kufanya ukaguzi nchi nzima ili kubaini ubadhilifu uliofanyika katika fedha za ruzuku ambazo zimekuwa zikagawiwa hata kwa watu waliofariki dunia”, alisisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amevipongeza vyombo vya habari nchini na kuvitaka kuendelea kuzitangaza juhudi za serikali na kuvitaka kutoa elimu bila kupotosha kwa vile maendeleo hayana chama ni lazima Watanzania wote washikamane katika suala la maendeleo.

Naye, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamini William Mkapa aliyekuwa Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo alishukuru  Mfuko wa dunia wa kupambana magonjwa ya  kifua kikuu, ukimwi na malaria kwa kushirikiana na Serikali na Taasisi yake kwa miaka 14 na kuiomba kuendelea kushirikiana na wadau wengine wanaopingana na maradhi ikiwemo Taasisi ya Mkapa.

Naye, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema Serikali inadhamiria kuwa ifikapo mwaka 2020 asilimia 60 ya Watanzania wapate huduma ya afya kupitia bima za afya hiyo kubadili hali ya sasa ambapo ni asilimi 28 ndio wanapata huduma hiyo nchini.

[caption id="attachment_6088" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wakati Mbunge wa Chato ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani alipokuwa akihutubia wananchi wa Chato mkoani Geita.[/caption]

Alisema aliseama kuwa Wizara yake ni kati ya Wizara zilizotengewa bajeti kubwa kwa mwaka 2017/2018  kupitia fedha hizo wataboresha huduma za Afya nchini ikiwa ni kuimaimarisha  huduma na afya ya  mama na mtoto na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Alieleza kuwa kwa mwaka huu tWizara itaboresha vituo vya afya 170 nchini, kujenga benki za damu katika mikoa 10 na kujitahidi kuhakikisha kuwa hakuna mwanamke atakayefariki kwa sababu ya kuvuja damu na kukosa dawa ya kuzuia ya kifafa cha mimba na kwamba Serikali itatoa dawa za kuongeza damu.

Aidha, alisisitiza kuwa bado sekta ya afya inakabiliwa na uhaba wa watumishi wa afya na kutolea mfano hospitali ya Chato pekee kukabiliwa uhaba wa watumishi kwa asilimia 45, huku akiwataka viongozi wa hospitali za mikoa kusimamia vizuri matumizi ya dawa.

[caption id="attachment_6091" align="aligncenter" width="750"] Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chato Shaaban Ntarambe hati ya kituo cha kukamua Mafuta ya Alizeti (Double Refine) kilichojengwa Chato mkoani Geita kwa Msaada wa Serikali ya[/caption]

Taasisi ya Benjamini Mkapa ilianzishwa mwaka 2005 ambayo imekuwa  ikitoa huduma maeneo ya vivjijini ambapo imejenga nyumba za watumishi 450 nchi nzima huku ikilenga kujenga nyumba 480, tangu mwaka 2011 imetoa  ajira 1,100 kwa wataalamu wa afya  na kufundisha vyuo  43 nchini .

Taasisi hiyo imetoa ufadhili kwa wanafunzi 949 wanaosomea maswala ya afya, huku 826 wakisubiri ajira katika taasisi za sekta hiyo sambamba na kujenga vituo 11 vya upasuaji nchini.

Ujenzi huo wa nyumba 50 umegharimu shilingi bilioni 2.5. na kutekelezwa kwa kutumia wakandarasi wa Kitanzania. Mpaka sasa Taasisi ya Mkapa imejenga zaidi ya nyumba 400 katika mikoa 17 nchini, kufanya ukarabati na ujenzi wa nyumba za waguzi wa sekta ya afya.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi