Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, Kamishna Jenerali wa Magereza CGP Suleiman Mzee pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu vya Vyombo vya Ulinzi na Usalama, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa nyumba 24 za makazi ya Maafisa na Askari Magereza katika eneo la Gereza la Isanga mkoani Dodoma leo tarehe 04 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua nyumba hizo za mpya za Maafisa na Askari Magereza katika eneo la Gereza la Isanga mkoani Dodoma leo tarehe 04 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mhandisi Bonanza Marata kuhusu mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha Samani cha Jeshi la Magereza mkoani Dodoma kabla ya kuweka jiwe la msingi leo tarehe 04 Januari 2021 katika eneo la Msalato
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli akikagua na Kuendesha magari mapya ya Jeshi la Magereza nchini mara baada ya kufungua Majengo ya Makao Makuu ya Jeshi hilo Msalato mkoani Dodoma.
Taaswira ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza yaliyopo Msalato mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akikagua baadhi ya Mashine ambazo zimeanza kufungwa katika Kiwanda hicho cha Samani cha Magereza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Maafisa na Askari Magereza mara baada ya kufungua Majengo ya Makao Makuu ya Jeshi hilo Msalato mkoani Dodoma.