Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu ya na Mafunzo Stadi (VETA), Bw. Peter Maduki baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) cha mkoa wa Kagera eneo la Burugo nje kidogo la mji wa Bukoba leo Jumatatu Januari 18, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kufungua Majengo ya mapya ya madarasa ya Shule ya Sekondari ya wavulana ya Ihungo iliyopo Bukoba mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akipeana mikono na Balozi wa Uingereza hapa nchini
David Concar alipomaliza kuongea na wananchi baada ya kufungua Majengo ya mapya ya madarasa ya Shule ya Sekondari ya wavulana ya Ihungo iliyopo Bukoba mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo wakati akielezea kuhusu ujenzi wa Majengo Mapya ya Shule hiyo ya Ihungo Sekondari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Balozi wa Uingereza hapa nchini David Concar, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti wakati akikata utepe kufungua Majengo mapya ya madarasa ya Shule ya Sekondari Ihungo ambayo iliathiriwa vibaya na tetemeko la Ardhi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua madarasa ya Shule ya Sekondari ya Ihungo ambayo ilijengwa upya mara baada ya tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016 mkoani Kagera.