Rais Dkt. Mwinyi Mwinyi Atembelea na Kukagua Ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Lumumba
Nov 19, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo ya ujenzi kutoka kwa Mshauri Elekezi wa Kampuni ya Habconsult Ltd, Arch. Habib Shariff Nuru.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akitembelea Ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi inayojengwa katika eneo la Lumumba Wilaya ya Mjini Unguja, akiwa katika ziara yake kutembelea ujenzi huo na kujionea hatua iliyofikia.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Nassor Ahmed Mazrui, wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa jengo jipya la Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, linalojengwa katika eneo la viwanja vya Lumumba Wilaya ya Mjini leo 19-11-2022.