Rais Dkt. Mwinyi Azungumza na Uongozi wa Taasisi ya Kidemokrasia Inayoshughulikia Masuala ya Kimataifa (NDI)
Sep 01, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa ripoti ya Sisi ni Wamoja, Mtazamo wa Wananchi Kuhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa, utafiti uliofanywa na Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar, akikabidhiwa na Rashid Azizi Rashid (kulia kwake), Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Bi. Salma Haji Saadat, baada ya kumaliza mazungumzo na uongozi wa Taasisi ya Kidemokrasia Inayoshughulikia Masuala ya Kimataifa (NDI) yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 1-9-2022
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Kidemokrasia Inayoshughulikia Masuala ya Kimataifa (NDI), Bi. Sandy Quimbaya, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 1-9-2022.