Rais Dkt. Mwinyi Azungumza na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa ya Oman
Aug 25, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Nyaraka na Kumbukumbu za Kitaifa ya Oman, Dkt. Hamed Mohd Al Dhawiani (kulia kwa Rais) alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 25-8-2022, akiwa na Balozi Mdogo wa Oman anayefanyia kazi zake Zanzibar, Mhe. Said Salim Al-sinawi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo ya moja ya kitabu kinachoelezea historia na kumbukumbu ya Oman na Zanzibar kutoka kwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Nyaraka na Kumbukumbu za Kitaifa ya Oman, Dkt. Hamed Mohd Al Dhawiani, wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 25-8-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Kitabu kinachoelezea historia ya Zanzibar na Oman na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Nyaraka na Kumbukumbu za Kitaifa ya Oman, Dkt. Hamed Mohd Al Dhawian, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 25-8-2022, na kulia kwake ni Balozi Mdogo wa Oman anayefanyia Kazi zake Zanzibar, Mhe. Said Salim Al Sinawi