Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Dkt. Mwinyi Azungumza na Mabalozi wa Tanzania Ikulu
Sep 05, 2023
Rais Dkt. Mwinyi Azungumza na Mabalozi wa Tanzania Ikulu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,walipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo 5-9-2023 kwa mazungumzo na kumuaga wakielekea katika vituo vyao vya Kazi walivyopangiwa, mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar,ujumbe huo ukiongozwa na Balozi wa Tanzania Nchini Canada, Mhe. Balozi Joseph Sokoine (kulia kwa Rais) na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said.
Na Ikulu - Zanzibar

Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) walipofika Ikulu jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kumuaga, mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo 5-9-2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 5-9-2023, walipofika kwa ajili ya mazungumzo na kumuaga wakielekea katika vituo vyao vya Kazi walikopangiwa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi