Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kulifungua Tawi la Benki ya CRDB Wete Pemba Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba na (kushoto kwa Rais) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela na (kulia kwa Rais) ni Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi. Ufunguzi huo wa Tawi la Benki ya CRDB ulifanyika leo 25-7-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi funguo ya Pikipiki (Bodaboda) Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Kaskazini Pemba, Ndg. Said Kassim Juma zilizotolewa kwa mkopo nafuu na Benki ya CRDB, wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Tawi la Benki hiyo Wete Pemba (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela na (kulia kwa Rais) ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe. Salama Mbarouk Khatib na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmaji Mussa Nekela akizunguma na kutoa maelezo kuhusiana na huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki yake kwa Wananchi, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Tawi la Benki hiyo Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, lililofunguliwa leo 25-7-2022, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika ziara yake Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika hafla ya ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB Wete Pemba leo 25-7-2022, wakati wa ziara yake katika Mkoa huo, kutembelea miradi ya maendeleo ya Mkoa huo