Rais Dkt. Mwinyi Azindua Muongozo wa Mafunzo ya Sayansi, Kingereza na Hisabati kwa Skuli za Sekondari Zanzibar
Aug 03, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Wageni waalikwa katika hafla ya Uzinduzi wa Muongozo wa Mafunzo ya Elimu ya Sayansi kwa Skuli za Sekondari Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati akihutubia na kizindua Muongozo huo, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 3-8-2022.
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuzindua Muongozo wa Mafunzo ya Sayansi kwa Skuli za Sekondari Zanzibar, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 3-8-2022
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Muongozo wa Mafunzo ya Sayansi kwa Skuli za Sekondari Zanzibar, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 3-8-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Vitabu vya Muongozo wa Mafunzo ya Sayansi, Hisabati na Kingereza na Balozi wa Korea ya Kusini Nchini Tanzania, Mhe. Sun Pyo Kim (kulia kwa Rais) na Mkurugenzi Mkaazi wa KOICA Tanzania, Bw. Kyucheol Eo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said na (kushoto kwa Rais) ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Mohammed Mussa, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Ali Abdulgulam Hussein.