Rais Dkt. Mwinyi Aweka Jiwe la Msingi Kituo cha Wajasiriamali Tumbe
Jul 27, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisoma maelezo ya Jiwe la Msingi la Kituo cha Wajasiriamali Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo hicho akiendelea na ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba kutembelea Miradi ya Maendeleo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyiakimsikiliza Mkuu wa Kikosi cha KMKM, Commodore Azana Hassan Msingiri akitoa maelezo ya Kituo cha Wajasiriamali Tumbe, wakati akitembelea Ujenzi huo baada ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi huo, na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe Masoud Ali Mohammed.
Wananchi wa Kijiji cha Tumbe Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Wananchi baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha Wafanyabiashara na Wajasiriamali Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba, wakati wa ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Mikoa Miwili ya Pemba.