Rais Dkt. Mwinyi Aweka Anwani ya Makazi katika Makazi yake Migombani
Aug 23, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiweka namba ya Anwani ya Makazi 78 Barabara ya Julius Nyerere katika Makazi yake Rais wa Zanzibar eneo la Migombani leo 22-8-2022, (kushoto kwa Rais) ni Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed, akitoa maelezo ya Anwani ya Makazi, baada ya uwekaji wa anwani hiyo uliofanyika leo 22-8-2022, katika Makazi ya Rais wa Zanzibar eneo la Migombani Wilaya ya Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali (hawapo pichani) baada ya uwekaji wa Anuwani ya Makazi ya Rais wa Zanzibar eneo la Migombani Wilaya ya Mjini na (kulia kwa Rais ) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Salum Mohammed