Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg, Saleh Juma Mussa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Ikulu, kabla ya Uteuzi alikuwa Afisa Mwandamizi Ofisi ya Rais Ikulu, hafla iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg, Thabit Idarous Faina kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Tume ya Uchaguzi,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg. Khamis Abdulla Saidi kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg. Maryam Juma A. Sadalla kuwa Katibu Mkuu (Kazi na Uwezeshaji) katika Ofisi ya Rais, Kazi,Uchumi na Uwekezaji kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, hafla iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg. Abeda Rashid Abdallah kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kabla ya Uteuzi huu alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto ,hafla ya kiapo imefanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
Viongozi Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama ni miongoni mwa waalikwa waliohudhuria katika hafla ya kiapo cha Viongozi walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi hivi karibuni katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman (kushoto) Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Hamid Mahmoud Hamid na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa wakiwa katika hafla ya kiapo kwa Viongozi walioteuliwa hivi karibuni, hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.