Rais Dkt. Mwinyi Ashiriki katika Mahafali ya 52 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Sayansi ya Bahari Buyu Zanzibar
Nov 14, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipohudhuria katika wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa mgeni rasmi katka duru ya nne ya mahafali ya 52 Taasisi ya Sayansi ya Bahari, Buyu Wilaya ya Magharibi "B" Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akifuatana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Viongozi wa Chuo hicho katika maandamano ya duru ya nne ya mahafali ya 52,yaliyofanyika leo,katika viwanja vya Taasisi ya Sayansi ya Bahari,Buyu Wilaya ya Magharibi "B" Unguja.
Baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Taasisi ya Sayansi ya Bahari, Buyu Wilaya ya Magharibi "B" Unguja wakiwa katika maandamano ya duru ya nne ya mahafali ya 52 yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) alipokuwa akimkabidhi cheti, Ndg. Kulwa Mtaki mara baada ya kutunukiwa Digirii ya Udaktari wa falsafa katika sayansi ya Bahari (Doctor of philosopony in Marine Sciences) ya Chuo Kikuu cha Dar es salam katika sherehe za mahafali ya 52,duru nya nne ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Taasisi ya Sayansi ya Bahari,Buyu Wilaya ya Magharibi "B" Unguja.
Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama ni Miongoni mwa waalikwa katika sherehe ya mahafali ya 52 duru nya nne ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Sayansi ya Bahari, Buyu Wilaya ya Magharibi "B" Unguja,yaliyofanyika leo ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani).
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akimtunuku Ndg.Mbiru Moses, Digirii ya Udaktari wa falsafa katika sayansi ya Bahari (Doctor of philosopony in Marine Sciences) ya Chuo Kikuu cha Dar es salam katika sherehe za mahafali ya 52 duru ya nne ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika leo viwanja vya Taasisi ya Sayansi ya Bahari, Buyu Wilaya ya Magharibi "B" Unguja. (kushoto) ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa mgeni rasmi wa mahafali hayo.
Wahitimu wa Digirii za Uzamivu, Umahiri na Awali wakila kiapo cha mara baada ya kutunukiwa shahada zao leo katika sherehe za mahafali ya 52, duru nya nne ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika leo viwanja vya Taasisi ya Sayansi ya Bahari, Buyu Wilaya ya Magharibi "B" Unguja, mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akitoa hutuba yake katika sherehe ya kuwatunuku Shahada wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Sayansi ya Bahari hafla iliyofanyika leo katika viwanja vya Taasisi hiyo Buyu Wilaya ya Magharibi "B" Unguja.