Rais Dkt. Mwinyi Amuapisha Katibu Mkuu Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko
Nov 24, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimshuhudia Ndg. Ali Khamis Juma, akitia saini hati ya kiapo baada ya kumuapisha kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ra Biashara Viwanda na Masoko ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, (katikati) ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi hati ya kiapo Ndg. Ali Khamis Juma, baada ya kumuapisha kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar,kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali (katikati) ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said.