Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuweka Jiwe la Msingi la Kiwanda cha Maji cha Watercom Kinyikani Mchangamdogo Pemba (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwa Rais) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe .Omar Said Shaban, hafla hiyo imefanyika katika kiwanda hicho ikiwa ni shamrashamra za kusherehekekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe, Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Bi. Maryam Omar, akitoa matatizo ya maradhi ya mtoto wake Aisha Ali Mussa (10) baada ya kumaliza hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la kiwanda cha maji katika kijiji cha kinyikani mchangamdogo Mkoa wa Kaskazini Pemba
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe. Omar Said Shaban akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuzungumza na Wananchi wakati hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la kiwanda cha maji safi cha Watercom Kinyikani Mchangamdogo Pemba
Mwakilishi wa Jimbo la Kojani Pemba, Mhe. Hassan H. Omar, akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la kiwanda cha maji cha Watercom kinachojengwa katika Kijiji cha Kinyikani Mchangamdogo Pemba, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Viongozi na Wananchi Kisiwani Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la kiwanda cha maji cha Watercom kinachojengwa na muwekekezaji katika Kijiji cha Kinyikani Mchangamdogo Pemba, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwakilishi wa Kampuni ya Watercom Ndg. Abubakary Ally akitoa maelezo ya ujenzi wa kiwanda cha Maji Safi cha Watercom, baada ya kuweka Jiwe la Msingi, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na (kulia kwa Rais) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe.Omar Said Shaban, hafla hii imefanyika katika eneo la kiwanda hicho Kijiji cha Kinyikani Mchangamdogo Mkoa wa Kaskazini Pemba.