Rais Dkt. Mwinyi Akutana na Kuzungumza na Balozi Dkt. Suleiman Haji Suleiman na Kamishna wa Polisi
Aug 04, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Nchini Marekani, Mhe Suleiman Haji Suleiman baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar, alipofika kujitambulisha leo 4-8-2022
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiagana na Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Nchini Marekani, Mhe. Suleiman Haji Suleiman baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 4-8-2022
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamad Khamis Hamad alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 4-8-2022
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiagana na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamad Khamis Hamad baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 4-8-2022, alipofika kujitambulisha.