Rais Dkt. Mwinyi Ahutubia Maadhimisho ya Miaka Miwili ya Uongozi Wake
Nov 09, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa na Wananchi wa Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika maadhimisho ya miaka miwili ya uongozi wake, yaliyofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba 8-11-2022
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi akijumuika na Wananchi na Viongozi wa Serikali wakati Kikundi cha Taarab cha Wajelajela wakitoa burudani katika Maadhimisho ya Miaka Miwili ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, iliyofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba 8-11-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyiakikabidhiwa zawadi ya picha ya kuchora na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe. Zahro Mattar Masoud, wakati wa Maadhimisho ya miaka miwili ya uongozi wake, yaliyofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba 8-11-2022.
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakishangilia na kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi. (hayupo pichani) wakati akihutubia katika Maadhimisho ya miaka miwili ya uongozi wake yaliyofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba 8-11-2022.