Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika matembezi ya Ufunguzi wa Wiki ya Sheria Tanzania inayofanyika Jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma na (kushoto kwa Rais) Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof Ibrahim Hamis Juma na Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla na (kulia kwa Rais) Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe Dkt. Tulia Ackson, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Anthony Mtaka, wakishiriki katika matembezi hayo yalioazia Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma na kumalizika katika viwanja vya Nyerere Square Dodoma leo 23-1-2022
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akitembelea maonesho ya Ufunguzi wa Wiki ya Sheria Tanzania, katika banda la Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mradi, Bi. Asha Hassan Komba na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof Ibrahim Hamis Juma, maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akitembelea banda la maonesho la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bw. Stanislaus Kagisa na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Boniface Simbachawene
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipandisha bendera ya Mahakama Kuu Tanzania katika hafla ya Ufunguzi wa Wiki ya Sheria iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma, na (kushoto kwa Rais) Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe.Dkt. Tulia Ackson.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiondoa kipazia kuashiria kuizindua Nembo ya Mahakama Kuu Tanzania wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria Tanzania iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof.Ibrahim Hamis Juma
Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia na kufungua Wiki ya Sheria Tanzania iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.