Rais Dkt. Mwinyi Afungua Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Afrika
Jul 12, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe Haroun Ali Suleiman akitoa maelezo kuhusiana na mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Afrika, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahri Mbweni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja uliofanyika leo 12-7-2022
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Viongozi Wakuu wa Serikali baada ya kuwasili katika ukumbi wa Madinat Al Bahri Mbweni, wakati ukipigwa wimbo wa Taifa na wa Afrika Mashariki, kabla ya kuanza kwa ufunguzi wa mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Afrika, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahri Mbweni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 12-7-2022.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Afrika, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt, Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia na kuufungua mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahri Mbweni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 12-7-2022
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Afrika, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 12-7-2022
Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA, Ahmed Khamis Makarani akizungumza na kutoa maelezo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Afrika, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahri Mbweni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 12-7-2022