Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Cheti cha udhamini Meneja Uhusiano Bima Benki ya CRDB – Zanzibar, Bi. Hamida Juma, wakati wa hafla ya ufunduzi wa mkutano wa Mjadala wa Uwekezaji wa Big Breakfast, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Tuzo Maalum ya Kuhamasisha Uwekezaji Zanzibar Namba Moja, akikabidhiwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mjadala wa Uwekezaji wa Big Breakfast, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akifuatilia mjadala kuhusiana na Fursa ya Uwekezaji Zanzibar, ikiwasilishwa mada hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Zanzibar, Ndg. Sharif Ali Sharif (hayupo pichani) na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Zanzibar
Washiriki wa Mjadala wa Uwekezaji wa Big Breakfast wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kufungua Mjadala wa Uwekezaji wa Big Breakfast uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.