Rais Dkt. Mwinyi Afungua Kituo cha TEHAMA Bwefum Unguja Wilaya ya Magharibi "B"
Oct 26, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Kituo cha Tehama Bwefum Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo tarehe 26-10-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kukifungua Kituo cha TEHAMA, Bwefum Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo tarehe 26-10-2022 na (kushoto kwa Rais) ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Tanzania, Mhe. Nape Nnauye na (kulia kwa Rais) ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Tanzania, Bi. Joustine Tmashiba, wakati akitembelea Kituo cha TEHAMA baada ya kukifungua leo 26-10-2022, katika eneo la Bwefum Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Tanzania, Mhe. Nape Nnauye akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Kituo cha TEHAMA Bwefum Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo tarehe 26-10-2022, kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Tehama Bwefum Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo tarehe 26-10-2022.