Rais Dkt. Mwinyi Afungua Kikao cha Dharura cha Baraza la Vyama vya Siasa
Jul 21, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo ni miongoni mwa wajumbe wa kikao cha siku mbili cha dharura cha Baraza la Vyama vya Siasa kilichofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani)katika ukumbi wa Madinat Al Bahr Hotel nje ya Jiji la Zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama cha Siasa cha wakulima (AAFP), Mhe. Sais Sudi Said alipokuwa akijitambulisha katika kikao cha dharura cha siku mbili chaBaraza la Vyama vya Siasa kilichofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani)katika ukumbi wa Madinat Al Bahr Hotel nje ya Jiji la Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake ya Ufunguzi wa kikao cha siku mbili cha dharura cha Baraza la Vyama vya Siasa kilichoanza leo katika ukumbi wa Madinat Al Bahr Hotel nje ya Jiji la Zanzibar.