Rais Dkt. Mwinyi Aendelea na Ziara yake Mkoa wa Kusini Unguja
Jul 22, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Baadhi ya Watendeji wa Mkoa wa Kusini Unguja wakifuatilia taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Mkoa huo wakati ikiwasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Rashid Hadih Rashid katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo 22-7-2022.
Baadhi ya Mawaziri na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa Kazi za Maendeleo za Mkoa ikisomwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadid Rashid, katika ukumbi wa Ofisi ya Mkoa Tunguu leo 22-7-2022 kabla ya kuanza kwa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja leo 22-7-2022
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Rashid Hadid Rashid akisoma taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Mkoa wake, kabla ya kuanza kwa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Wilaya ya Kusini Unguja leo 22-7-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mhandisi wa Wizara ya Afya Zanzibar, Said Ali Bakar akitoa maelezo ya michoro ya jengo jipya la Hospitali ya Wilaya Kitogani Wilaya ya Kusini Unguja, wakati wa ziara yake katika Wilaya hiyo kutembelea Miradi ya Maendeleo, hospitali hiyo inayojengwa kwa fedha za Uviko-19, na (kushoto kwa Rais) ni Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na (kulia kwa Rais) ni Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe Hassan Hafidh Khamis.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kusini inayojengwa Kitongaji kupitia Fedha za Uviko-19, akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Kusini Unguja leo 22-7-2022, na (kushoto kwa Rais) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman.