Rais Dkt. Mwinyi Aelekea Nchini Oman kwa Ziara ya Kikazi ya Siku Nne
Oct 11, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakisalimiana na kuagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akielekea nchini Oman kwa ziara ya siku nne ya kikazi nchini humo leo tarehe 11-10-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akielekea nchini Oman kwa ziara ya kikazi ya siku nne nchini humo leo 11-10-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwapungia mkono na kuwaaga viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Siasa, wakati akiondoa nchini kuelekea nchini Oman kwa ziara ya kikazi ya siku nne nchini humo leo 11-10-2022.