Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Dkt. Magufuli Apokea Hati za Utambulisho za Mabalozi 5
Aug 29, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_46369" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Mhe. Sanjiv Kohli Balozi wa India hapa nchini Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_46370" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Denmark hapa nchini Mhe. Mette Norgaard Dissing Spandet Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Agosti, 2019 amepokea hati za utambulisho za Mabalozi 5 walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi hao ni Mhe. Mahayub Buyema Mahafud (Balozi wa Jamhuri ya Saharawi hapa nchini), Mhe. Sanjiv Kohli (Balozi wa India hapa nchini), Mhe. Mej. Jen. Anselem Nhamo Sanyatwe (Balozi wa Jamhuri ya Zimbabwe hapa nchini), Mhe. Sandro Renato Agostinho De Oloveira (Balozi wa Jamhuri ya Angola hapa nchini) na Mhe. Mette Nørgaard Dissing Spandet (Balozi wa Denmark hapa nchini).

Katika mazungumzo, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza na kuwakaribisha Mabalozi hao hapa nchini Tanzania, na kuwahakikishia kuwa Tanzania inatambua uhusiano na ushirikiano mzuri na wa kihistoria na nchi zao na kwamba ipo tayari kuukuza na kuuimarisha zaidi uhusiano huo.

[caption id="attachment_46371" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Mhe. Meja Jenerali Anselem Nhamo Sanyatwe Balozi mteule wa Zimbabwe hapa nchini Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_46372" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Angola hapa nchini Mhe. Sandro Renato Agostinho De Oliveira mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption]

Mhe. Rais Magufuli amewataka Mabalozi hao kuungana na Tanzania katika juhudi kubwa za kuleta mageuzi ya kiuchumi na amewaomba wawaalike wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi zao kuwekeza Tanzania halikadhalika wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania kwenda kuwekeza katika nchi hizo.

Ametaja baadhi ya fursa zilizopo Tanzania kuwa ni ujenzi wa viwanda, ardhi kwa ajili ya kilimo na ufugaji, soko la uhakika na uwekezaji katika sekta ya gesi na mafuta.

Mabalozi hao wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kukaribishwa Tanzania na wameahidi kufanya juhudi kubwa za kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na nchi zao katika nyanja mbalimbali hasa uchumi na huduma za kijamii.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

29 Agosti, 2019

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi