Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Dkt. Magufuli Amuapisha Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Jun 06, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_2824" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Juni, 2017 amemuapisha Bibi Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Bibi Anna Elisha Mghwira amejaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Saidi Meck Sadiki aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo.

Hafla ya kuapishwa kwa Bibi Anna Elisha Mghwira imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

[caption id="attachment_2827" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakishuhudia tukio hilo Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_2828" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akisaini Hati ya Kiapo cha Udilifu kwa Viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption]

Akizungumza baada ya kumuapisha, Mhe. Rais Magufuli amemtaka Bibi Anna Elisha Mghwira kwenda kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kuondoa kero zinazowakabili wananchi wa Kilimanjaro bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa, dini, makabilia na kanda wanazotoka.

Mhe. Rais Magufuli amemhakikishia kuwa atapata ushirikiano wa kutosha wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake na asikubali kuyumbishwa na mtu yeyote katika majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.

[caption id="attachment_2829" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akizungumza mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_2830" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_2833" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_2836" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na viongozi wengine Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_2839" align="aligncenter" width="750"] Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira huku Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi pamoja na wakuuu wa Wilaya za Ubungo na Ilala wakipiga makofi.[/caption]

Mimi huwa siteui watu hivi hivi, huwa naangalia uwezo wa mtu, na wewe nimekuchunguza na nimejiridhisha kuwa una uwezo wa kuwatumikia wananchi, nenda kachape kazi, kawaondolee kero wananchi wa Kilimanjaro, wapo watu watakaokusema na wengine watakuonea wivu, wewe kachape kazi amesema Mhe. Rais Magufuli.

Kwa upande wake Bibi Anna Elisha Mghwira amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na amemuahidi kuwa yupo tayari kwenda kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kujenga Taifa.

“Ninasema hii ni heshima kwa Taifa letu, ni heshima kwa umoja wa nchi yetu, ni heshima kwa siasa za umoja wa nchi yetu, kumekuwa na minong’ono mingi sana kuwa Rais analeta nini, kuteua watu wanaitwa wapinzani, mimi sio mpinzani wa maendeleo” amesema Bibi Mghwira.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

06 Juni, 2017

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi