[caption id="attachment_24824" align="aligncenter" width="800"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Magufuli akizungumza na wananchi na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakati wa uzinduzi wa mradi wa nyumba za makazi zilizojengwa na Shirika hilo katika eneo la Iyumbu mkoani Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_24825" align="aligncenter" width="800"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Magufuli akizindua mradi wa nyumba za makazi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika eneo la Iyumbu mkoani Dodoma.[/caption]
Frank Mvungi – Maelezo, Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amerejesha kwa wananchi eneo lenye ukubwa wa ekari 129 ililokuwa limechukuliwa na Serikali kwa ajili ya makaburi ya Viongozi wa Serikali lililopo kijiji cha Iyumbi, Dodoma ili walitumie kwa shughuli za uzalishaji na kijiinua kiuchumi.
Akizungumza wakati akizindua mradi wa nyumba (Iyumbi Satelite Center) wenye nyumba 300 ambapo 150 kati ya hizo zimeshakamilika, Dkt. Magufuli amesema mradi huo unaoteklezwa na Shirikika la Nyumba la Taifa (NHC) makazi bora watumishi wa umma wanaohamia Dodoma kwa kuwa nyumba hizo ni za gharama nafuu.
“Nawapongeza NHC kwa kazi nzuri na kutekeleza kwa vitendo dhamira ya kuwa na makazi bora kwa wananchi kwa kujenga nyumba hizi za Iyumbu wenye thamani ya Bilioni 13 ”, alisisitiza Dkt. Magufuli
[caption id="attachment_24826" align="aligncenter" width="800"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Magufuli akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bi.Blandina Nyoni na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw.Nehemia Mchechu wakati wa uzinduzi wa mradi wa nyumba za makazi zilizojengwa na Shirika hilo katika eneo la Iyumbu mkoani Dodoma.Naye Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu amesema kuwa licha kuwa na mradi huo utakaokuwa na nyumba 300 , Shirika hilo litatekeleza mradi mwingine katika eneo la Msalato mjini Dodoma.
Aliongeza kuwa Shirika hilo limejipanga kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kujenga nyumba za gharama nafuu ili kuendana na Kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Shirika la Nyumba la Taifa limekuwa likitekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa Nyumba zikiwemo za gharama nafuu , Kati na Juu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na makazi Bora, Ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu ni moja ya hatua hizo ambapo 150 kati ya hizo zimeshakamilika.