Rais Dkt. Hussein Mwinyi Amuapisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar
Feb 25, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Kanali Burhan Zuberi Nassor kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 25-2-2022.
Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakifuatilia kuapishwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar, Kanali Burhan Zuberi Nassor akiapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani), hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 25-2-2022
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Othman Masoud Othman, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zuberi Ali Maulid, Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe.Idrissa Mustafa Kitwana wakifuatilia kuapishwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar. Kanali Burhani Zuberi Nassor, akiapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi. (hayupo pichani) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.