Rais Dkt. Hussein Mwinyi Akutana na Wajumbe wa Bodi ya BOT
Nov 07, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesa Florens Luoga (kulia kwa Rais) alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo akiwa na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa BOT na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa BOT wakiongozwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesa Florens Luoga (kulia kwa Rais) walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 7-11-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesa Florens Luoga, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 7-11-2022.