Rais Dkt. Hussein Mwinyi Afungua Mkutano wa Saba wa Pan African Humanitarian &Investment Summit Zanzibar 2022
Nov 08, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
WashirikI wa Mkutano wa saba wa Pan African Humanitarian & Investment Summit Zanzibar 2022 wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Wilaya ya Magharibi “B” leo 8-11-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi Maalum kutoka Serikali ya Seychelles akikabidhiwa na Rais Mstaafu wa Seyshelles, Mhe. Danny Faure, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa saba wa Pan African Humanitarian & Investment Summit Zanzibar 2022, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Wilaya ya Magharibi “B” leo 8-11-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum ya mfano wa Samaki na Balozi wa Heshima wa Seychelles Nchini Tanzania, Mhe. MaryVonne Pool, baada ya kuufungua wa mkutano wa saba wa Pan African Humanitarian &Investment Summit Zanzibar 2022, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Wilaya ya Magharibi “B” leo 8-11-2022.