Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Jukwaa Lajadili Usimamizi wa Maafa Nchini
Jan 22, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_27634" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustine Kamuzora akizungumza alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kikao cha kwanza cha Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa leo Jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo limejumuisha wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na sekta binafsi ambao kwa namna moja wanajishughulisha na masuala ya kukabiliana na maafa na majanga.[/caption]

Na: Jacquiline Mrisho

Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa limefanya mkutano wake wa kwanza wa kujadili masuala mbalimbali yaliyokuwa yakitekelezwa na wadau wake kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa maafa nchini.

Mkutano huo umefunguliwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Prof. Faustine Kamuzora ambaye amewasisitiza wadau wa jukwaa hilo kuwa na ushirikiano katika kutafuta njia mbadala za kukabiliana na maafa.

[caption id="attachment_27635" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maafa Ukanda wa Afrika (UNISDRI) Julius Kabubi akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha kwanza cha Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa leo Jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo limejumuisha wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na sekta binafsi ambao kwa namna moja wanajishughulisha na masuala ya kukabiliana na maafa na majanga.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Bashiru Taratibu, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bigedia Jenerali Mstaafu Mbazi Msuya na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustine Kamuzora.[/caption] [caption id="attachment_27636" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bigedia Jenerali Mstaafu Mbazi Msuya akielezea jambo wakati wa ufunguzi wa kikao cha kwanza cha Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa leo Jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo limejumuisha wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na sekta binafsi ambao kwa namna moja wanajishughulisha na masuala ya kukabiliana na maafa na majanga.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo Bashiru Taratibu, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustine Kamuzora na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maafa Ukanda wa Afrika (UNISDRI) Julius Kabubi.[/caption]

Prof. Kamuzora amesema kuwa mkutano huo utachangia kikamilifu mwanzo wa zama mpya za jukwaa hilo pia utaongeza kujitolea kwa Wizara, Idara na Mashirika, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Taasisi za Elimu, dini, asasi za kiraia, sekta binafsi na vyombo vya habari katika shughuli za usimamizi wa maafa.

“Jukwaa hili linakutana kwa mara ya kwanza tangu Sheria ya Usimamizi wa Maafa Namba 7 ya mwaka 2015 ianze kutumika, chombo hiki ni muhimu kwa ajili ya ushauri kwenye maeneo ya kipaumbele katika usimamizi wa maafa kwa uratibu na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali hivyo tunaamini kupitia nyie tutaimarisha usimamizi wa maafa nchini,” alisema Prof. Kamuzora.

Katibu Mkuu amefafanua kuwa kupunguza madhara ya maafa ni suala mtambuka linalohitaji utashi na kuwajibika kisheria, uelewa wa umma, elimu ya kisayansi pamoja na ufanisi wa utekelezaji wa sera hivyo jukwaa hilo lenye wataalam kutoka sekta mbalimbali litasaidia kuleta ujuzi na  rasilimali zinazohitajika katika upunguzaji wa madhara ya maafa.

[caption id="attachment_27637" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustine Kamuzora akimsikiliza kwa makini Mwanzilishi wa Taasisi ya Sukos DM Kova Foundation ambaye pia ni Kamishna mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova walipokutana katika kikao cha Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa leo Jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo limejumuisha wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na sekta binafsi ambao kwa namna moja wanajishughulisha na masuala ya kukabiliana na maafa na majanga.Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Bashiru Taratibu, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bigedia Jenerali Mstaafu Mbazi Msuya.[/caption] [caption id="attachment_27639" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustine Kamuzora akiteta akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kikao cha Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa leo Jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo limejumuisha wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na sekta binafsi ambao kwa namna moja wanajishughulisha na masuala ya kukabiliana na maafa na majanga. (Picha na: Frank Shija)[/caption]

Prof. Kamuzora ameyataja baadhi ya baadhi ya maeneo yatakayojadiliwa na jukwaa hilo yakiwemo ya Mkakati wa Upunguzaji wa Madhara ya Maafa wa Sendai 2015 – 2030, Mkakati na Mpango wa Usimamizi mto Msimbazi, Sheria ya Usimamizi wa Maafa na Kanuni za zake za Mwaka 2017, Rasimu ya Sera ya Taifa Usimamizi wa Maafa pamoja na Taarifa ya Jukwaa la Tano la Kimataifa la Kupunguza Madhara ya Maafa.

Masuala mengine yatakayojadiliwa ni Taarifa ya awali ya tathmini ya kina ya majanga, uwezekano wa kutokea, makadirio ya madhara na ramani katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma, maandalizi ya mkakati wa kujiandaa na kukabiliana na tetemeko la ardhi nchini pamoja na usimamizi wa Kituo cha Oparesheni na Mawasiliano ya Dharura na Mfumo wa Kidunia wa Huduma za Hali ya Hewa.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mstaafu wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ambaye pia anamiliki Taasisi inayohusika na kupambana na majanga ya maafa inayojulikana kama ‘Sukos Kova Foundation amesema kuwa jukwaa hilo limewakutanisha wadau mbalimbali watakaobadilishana mawazo na uzoefu ili waweze kuisaidia nchi ya Tanzania pamoja na nchi zingine katika kupambana na maafa kabla, wakati na baada ya kutokea kwa matukio hayo.

Jukwaa la Usimamizi wa Maafa limeundwa kwa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Namba 7 ya mwaka 2015 ikiwa na wajibu mkubwa wa kutathmini na kutoa ushauri wa kitaalam kwa Serikali kuhusu majanga ya aina zote.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi