Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Prof. Mkenda: Watanzania Tuwe Wazalendo Kununua Bidhaa Zetu
Jul 02, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na Ismail Ngayonga

WATANZANIA wametakiwa kuwa Wazalendo kwa kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa nchini ili kuwawezesha wazalishaji wa ndani hususani  wajasiriamali wadogo kuchangia kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa kati kupitia viwanda.

Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji) Prof. Adolf Mkenda wakati alipokuwa akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Ngozi katika katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF).

[caption id="attachment_5111" align="aligncenter" width="750"]  Baadhi ya mitambo na magari yanayotarajiwa kuzalishwa nchini na kampuni ya GF Truck and Equipement yakiwa katika sehemu ya bidhaa zinazopatikana katika maonesho ya Sabasaba.(Picha na: Frank Mvungi)[/caption]

Prof. Mkenda alisema Serikali ya Awamu ya Tano imekusudia kujenga mazingira mazuri kwa wazalishaji wadogo, hivyo ni wajibu wa Watanzania kujitokeza na kununua bidhaa zinazozalishwa nchini ili ziweze kufahamika katika masoko ya kimataifa.

“Tutaendelea kuwahamasisha wazalishaji wa bidhaa za ngozi kuongeza ubunifu zaidi ikiwemo kuwa kuweka chapa maalum katika bidhaa zao, hatua itayosaidia bidhaa zao ziweze kufahamika zaidi kwani bidhaa wanazozalisha tumezigundua kuwa zina ubora mzuri zaidi” .

Aliongeza kuwa hivi karibuni Serikali kupitia Mfuko wa Pesheni wa Mashirika ya Umma (PPF) umesaini mkataba na Gereza la Karanga kwa ajili ya kuzalisha sori za viatu ili kuhakikisha kuwa malighafi muhimu za bidhaa za uzalishaji wa viatu zinaweza kupatikana nchini badala ya kuagiza ncje ya nchi.

[caption id="attachment_5112" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (BiasharanaUwekezaji), Prof. Adolf Mkenda akitazama baadhi ya bidhaa za ngozi zinazozalishwa nchini wakati wa maadhimisho ya siku ya ngozi iliyofanyika katika viwanja vya maonesho ya biashara ya kimataifa Dar es Salaam. Wa kwanza Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Edwin Rutageruka.[/caption]

Profesa Mkenda alisema katika kuhakikisha kuwa wazalishaji wa bidhaa za ngozi wanapata tija na kuchangia kikamilifu katika uchumi wa nchi, Serikali kupitia Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam kampasi ya Mwanza kimekusudia kutoa masomo katika tasnia ya ngozi ili kuwawezesha kuwa na kiwanda cha pamoja cha uzalishaji wa bidhaa hizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka, alisema Serikali imekusudia kuwawezesha wazalishaji wa bidhaa za ngozi nchini wanakuwa na soko la pamoja ili kuhakikisha wanapata faida kutokana na uzalishaji wa bidhaa zao.

Alisema Serikali imeendelea na jitihada mbalimbali katika kuhakikisha kuwa wazalishaji wa bidhaa za ngozi wanaweza kupanua wigo wa biashara hiyo kufikia kiwango cha kimataifa, ambapo tayari wamewazesha wazalishaji wa bidhaa hizo katika mikoa ya Dodoma, Kilimanjaro na Dar es Salaam kupata mafunzo mbalimbali yaliyokusudia kuwaongezea ujuzi na maarifa katika uzalishaji wao.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Edwin Rutageruka akizungumzia mikakati ya Tantrade kuwawezesha wajasiriamali wanaozalisha bidhaa za ngozi nchini ikiwemo kuwapatia banda maalum la kuweka na kuuza bidhaa zao kwa kipindi cha mwaka mzima bila malipo.

Alisema TanTrade imekusudia kuwawezesha wazalishaji wa bidhaa za ngozi kuwa na soko la pamoja kwa kuwapatia banda la kuuza bidhaa zkwa kipindi cha mwaka mzima bila ya malipo ili kuwawezesha kuzalisha ajira kwa Watanzania wengi zaidi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi Nchini (TALEPA), Dedan Munisi aliiomba Serikali kufanya mazungumo na Taasisi za kifedha ikiwemo mabenki ili kuweza kuwatengea dirisha maalum la mikopo kwa wazalishaji wa bidhaa za ngozi nchini ili kubabiliana na changamoto ya mitaji inayowakabili wazalishaji mbalimbali nchini.

Aidha Munisi aliongeza kuwa Serikali haina budi kutoa kipaumbele cha kipekee kwa wazalishaji wa bidhaa za ngozi  nchini ili kuwawezesha kuwa kujenga imani na kujiamini katika uzalishaji wa bidhaa zao nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi