Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Prof. Kabudi: Hakuna Mgongano wa Kimamlaka katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar
Feb 06, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_28601" align="aligncenter" width="829"] Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akionesha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar wakati akitoa ufafanuzi kuhusu mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yale ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mapema leo Bungeni.

[/caption] [caption id="attachment_28605" align="aligncenter" width="900"] Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama.[/caption]

Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA

Serikali imesema Kikatiba hakuna mgongano wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar unaosababisha ongezeko kubwa la kero za Muungano na mgongano wa kimamlaka baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi bungeni leo mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Wingi Mhe. Juma Kombo lililohusu mgongano wa Katiba hizo.

Prof Kabudi amesema kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka utaratibu mahususi wa kushughulikia tafsiri ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na utekelezaji wake inayobishaniwa kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

[caption id="attachment_28600" align="aligncenter" width="799"] Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelezo Bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni kuhusu mikakati ya Serikali katika kuimarisha utendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania ili itimize lengo la kuanzishwa kwake.[/caption]

“Hadi sasa hakuna upande wowote baina ya Serikali hizi mbili ambao unatafsiri tofauti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano au utekelezaji wake”

“Hivyo kwa kuzingatia kuwa hakuna mgongano wa Katiba kati ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Serikali haina sababu ya kuleta mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba ili kuondoa changamoto hiyo ambayo haipo” amefafanua Prof Kabudi.

Akizunguzmzia kuhusu mgongano wa kimamlaka Prof. Kabudi amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anamamlaka yote katika masuala yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Mjini Mary Chandanda kuhusu upandishwaji vyeo kwa Mahakimu na Watumishi wa Mahakama, Prof Kabudi amesema kuwa suala la kupandisha vyeo watumishi wenye sifa stahiki ni wajibu endelevu kwa Serikali.

“Mahakama ya Tanzania imekuwa ikichukua hatua kuwapandisha Mahakimu na Watumishi wa ngazi mbalimbali vyeo kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kisheria ikiwa ni pamoja na muda wa utumishi kazini, utendaji kazi, weledi na maadili pamoja na upatikanaj wa vibali kutoka Idara Kuu ya Utumishi” amesema Prof Kabudi.

[caption id="attachment_28602" align="aligncenter" width="783"] Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akifafanua kuhusu utekelezaji wa miradi ya Usambazaji Umeme Vijijini (REA) ambapo dhamira ya Serikali ni kufikisha umeme katika vijiji vyote nchini.
[/caption] [caption id="attachment_28603" align="aligncenter" width="900"] Wabunge wakifuatilia kikao cha 6 cha Bunge, mkutano wa 10 unaoendelea mjini Dodoma.[/caption]

Hata hivyo, Prof. Kabudi amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2012/2013 jumla ya Mahakimu na Wasaidizi wa Sheria wa Majaji 52 walipandishwa vyeo, mwaka 2013/2014 jumla ya watumishi 200 walipandishwa vyeo, mwaka 2014/2015 Mahakimu na Wasaidizi wa Sheria wa Majaji 22 na watumishi 686 walipandishwa vyeo na mwaka 2015/2016 Mahakimu na Wasaidizi wa Sheria 59 na watumishi 447 walipandishwa vyeo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi