[caption id="attachment_24967" align="aligncenter" width="750"] Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akimkabidhi cheti cha utendaji bora WP Nina Dachi wa kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni.[/caption]
Na. Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi nchini limewaonya baadhi ya watumishi wasio waaminifu wanaofanya kazi katika Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya wizi wa mafuta na miundombinu mbalimbali ya shirika hilo kuacha mara moja.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi, Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi Mwandamizi Patrick Byatao wakati wa hafla fupi ya kuwatunukia zawadi baadhi ya Askari waliofanya vizuri katika kuhakikisha usalama wa miundombinu ya shirika hilo ambapo baadhi yao walifanikiwa kuwakamata watumishi wa shirika hilo wakiiba mafuta.
Amesema katika siku za karibuni kumekuwa na matukio kadhaa ya watumishi wa shirika hilo wasio waaminifu ambapo wamekuwa wakilitia hasara shirika hilo jambo ambalo amesema wanaendelea kuimarisha usalama ili kuhakikisha kuwa wanawadhibiti.
[caption id="attachment_24968" align="aligncenter" width="750"] Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akimkabidhi cheti cha utendaji bora mmoja wa askari wa kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni.[/caption] [caption id="attachment_24969" align="aligncenter" width="700"] Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akimkabidhi zawadi ya jiko la gesi mmoja wa askari wa kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni.[/caption] [caption id="attachment_24970" align="aligncenter" width="700"] Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akikagua gwaride wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku askari waliofanya vizuri kwa mwaka 2017 katika kikosi hicho ambapo kwa kiasi kikubwa wamezuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA. (Picha na Jeshi la Polisi)[/caption]Byatao amesema Kikosi hicho kitaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara ili kuhakikisha wanakomesha tabia hiyo ambayo imekuwa ikidhoofisha utendaji wa TAZARA pamoja na kuitia hasara Serikali.
Akizungumzia utoaji wa zawadi hizo. Byatao amesema askari hao kumi wamefanya vizuri kwa kujituma katika kipindi cha mwaka 2017 hivyo kwa mujibu wa taratibu za Jeshi la Polisi ni vyema kuwazawadia ili kuongeza morali yao ya kazi na kuwafanya wengine kuendelea kujituma zaidi.
Kwa upande wake mmoja wa Askari waliopata zawadi baada ya kufanya vizuri WP Nina Dachi amewaasa askari wenzake kuendelea kufanya kazi kwa umakini ili kuhakikisha kuwa miundominu ya shirika hilo inakuwa salama wakati wote.