Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Mbalimbali Yanayoendelea Katika Kambi ya Matibabu JKCI
Nov 26, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_23497" align="aligncenter" width="750"] Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart - SACH) ya nchini Israel Katharina Schmitt akiangali jinsi moyo wa mtoto unavyofanya kazi (Echocardiogram) kwenye kambi ya matibabu na upimaji wa moyo kwa watoto inayoendelea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Kulia ni Afisa Muuguzi wa JKCI Pal Bhadreshwara na kushoto ni mama wa mtoto.[/caption] [caption id="attachment_23498" align="aligncenter" width="750"] Mama Judy Shore kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel akielezea jinsi Taasisi hiyo inavyotoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto na mafunzo kwa wafanyakazi wa kada ya afya hapa nchini katika mkutano na waandishi wa habari uliozungumzia kambi ya matibabu ya moyo ya bila kufungua kifua (Catheterization) inayoendelea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo hadi sasa jumla ya watoto 20 wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na hali zao zinaendelea vizuri.Kulia ni Daktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kutoka JKCI Peter Kisenge.[/caption] [caption id="attachment_23499" align="aligncenter" width="750"] Daktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akiongea na waandishi wa Habari kuhusu uhusiano wa Taasisi hiyo na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart- SACH) ya nchini Israel ambapo hadi sasa jumla ya watoto 40 wamefanyiwa upasuaji wa moyo bure nchini Israel. Kulia ni Simon Fisher na kushoto ni Mama Judy Shore wote kutoka SACH.[/caption] [caption id="attachment_23500" align="aligncenter" width="750"] Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart - SACH) ya nchini Israel Katharina Schmitt akiangali jinsi moyo wa mtoto unavyofanya kazi (Echocardiogram) kwenye kambi ya matibabu na upimaji wa moyo kwa watoto inayoendelea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Kulia ni Afisa Muuguzi wa JKCI Pal Bhadreshwara na kushoto ni mama wa mtoto.[/caption] [caption id="attachment_23502" align="aligncenter" width="750"] Watoto wakicheza wakati wakisubiri kwenda kufanyiwa kipimo kinachoangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiogram) katika kambi ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel. Jumla ya watoto 100 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi kati ya hao 60 ambao watakuwa na matatizo makubwa watapelekwa nchini Israel kwa ajili ya matibabu na 40 watatibiwa hapa nchini. (Picha na JKCI)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi