Ofisi ya Waziri Mkuu Yafanya Kikao na Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar
Oct 13, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu imepata ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar ambao umelenga katika kubadilishana uzoefu katika masuala ya kazi, maendeleo vijana, ukuzaji ajira na ustawi wa Watu wenye Ulemavu.
Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Dkt. Islam Salum wakati wa kikao cha Ushauriano baina ya ofisi hiyo na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Oktoba 13, 2022 Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Ugeni huo umeongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais anayesimamia masuala ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji. Katika kikao hicho, ofisi hizo zimedhamiria kushirikiana kwa karibu katika kutekeleza majukumu sambamba na kutoa huduma kwa wananchi kwa tija na ufanisi katika pande zote mbili za Muungano.
Aidha, katika kikao kazi hicho, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Kazi, Uchumi na Uwekezaji aliambatana na Kamishna wa Kazi – Zanzibar pamoja na Mkurugenzi wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSH) – Zanzibar.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Bw. Leonard Mchau (kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao cha Ushirikiano baina ya ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar kilichofanyika Oktoba 13, 2022, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Bw. Pascal Vyagusa (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu muundo wa majukumu ya Ofisi hiyo wakati wa kikao cha Ushirikiano baina ya ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar.
Kamishna wa Kazi Msaidizi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Bi. Lilian Francis (kushoto aliyesimama) akiwasilisha taarifa kuhusu shughuli zinazotekelezwa na Idara ya Kazi wakati wa kikao cha Ushirikiano baina ya ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar kilichofanyika Oktoba 13, 2022, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Bw. Rashid Maftah (kulia) akiwasilisha taarifa kuhusu shughuli zinazotekelezwa na kitengo hicho wakati wa kikao cha Ushirikiano baina ya ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar kilichofanyika Oktoba 13, 2022, jijini Dodoma.