Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Nyongo Aifungia Kampuni ya Uchakataji Madini Bati Isiyo na Leseni
Mar 01, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_29073" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Ujumbe wake, wakikagua Mgodi wa Madini ya Bati wa Hamad Mine Scale, uliopo eneo la Omukasheni, Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Februari 28 mwaka huu, akiwa katika ziara ya kazi.

[/caption] [caption id="attachment_29074" align="aligncenter" width="983"] Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (mwenye Kaunda Suti-mbele) na Ujumbe wake, baada ya kukagua Mitambo inayotumika kusaga mawe yenye Madini ya Bati (kulia) katika Mgodi wa Hamad Mine Scale, uliopo eneo la Omukasheni, Wilaya ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera, Februari 28 mwaka huu, akiwa katika ziara ya kazi.[/caption]

Na Veronica Simba – KAGERA

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amemwagiza mmiliki wa Kampuni inayochakata Madini Bati ya African Top Minerals iliyopo Kyerwa mkoani Kagera, Hassan Ibar, kutoendelea na kazi hiyo hadi pale atakapofuata taratibu za kuomba na kupatiwa leseni halali ya Serikali.

Alitoa agizo hilo jana Februari 28, alipotembelea na kukagua Kampuni hiyo akiwa katika ziara yake ya kazi mkoani Kagera.

Naibu Waziri alimwambia mmiliki huyo kuwa, Serikali inapenda wawekezaji wawepo ili pamoja na mambo mengine wasaidie upatikanaji wa ajira kwa wananchi lakini akaonya kwamba kamwe haitaridhia mtu yeyote kufanya uwekezaji pasipo kuwa na leseni halali itakayowezesha kutambuliwa na Serikali na kulipa kodi zote stahiki.

[caption id="attachment_29075" align="aligncenter" width="1018"] Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (katikati), akikagua madini ghafi ya Bati (aliyoshika mkononi) na kuzungumza na mmoja wa wamiliki wa Mtambo wa kuchakata Madini hayo, Hassan Ibar (kushoto), alipotembelea na kuukagua Mtambo huo unaomilikiwa na Kampuni ya African Top Minerals, wilayani Kyerwa, Mkoa wa Kagera, Februari 28 mwaka huu. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali Shaban Lissu.
[/caption] [caption id="attachment_29076" align="aligncenter" width="750"] Mmoja wa wamiliki wa Mtambo wa kuchenjua Madini ya Bati wa TanzaPlus Minerals, Salim Mhando (kushoto), akimwonesha Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa pili kutoka kushoto), moja ya mashine zinazotumika kuchakata Madini hayo. Naibu Waziri alitembelea na kukagua Mtambo huo uliopo Nyaluzumbulwa wilayani Kyerwa, Mkoa wa Kagera, Februari 28 mwaka huu.[/caption]

“Naomba utambue kuwa unafanya shughuli hii kinyume cha sheria. Hivyo naagiza, kuanzia sasa usiendelee na kazi hadi pale utakapokuwa na leseni.”

Aidha, Naibu Waziri pia alitembelea maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kyerwa kuliko na shughuli za uchimbaji madini ya Bati pamoja na Viwanda kadhaa vya uchakataji Madini hayo, vikiwemo vya TanzaPlus Minerals na Hamad Mine Scale.

Akizungumza na wana-kikundi wa Umoja wa Wachimbaji Kyerwa, Naibu Waziri aliwasihi wawe wavumilivu wakati Serikali ikishughulikia suala la kujisajili na Mikataba ya Kimataifa itakayowezesha kutambulika kwa Madini ya Bati yanayochimbwa nchini ili yaweze kuuzwa popote Duniani.

“Natambua mnapitia kipindi kigumu kutokana na zuio tuliloweka la kutouza Madini ghafi nje ya nchi. Serikali inashughulikia suala hilo kwa uharaka ili kama nchi, nasi tuweze kuingia katika Mikataba hiyo ya Kimataifa ambayo itatuwezesha kuleta wawekezaji mbalimbali hapa, waje wanunue madini yetu hapa kwa ushindani, na tuuze kwa bei nzuri zaidi tofauti na ilivyo sasa.”

[caption id="attachment_29077" align="aligncenter" width="813"] Madini ya Bati yaliyo ghafi.
[/caption] [caption id="attachment_29078" align="aligncenter" width="750"] Ujumbe wa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo wakikagua shimo linalochimbwa Madini ya Bati katika Mgodi wa Hamad Mine Scale, uliopo eneo la Omukasheni, Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Februari 28 mwaka huu, akiwa katika ziara ya kazi.[/caption]

Hata hivyo, Naibu Waziri aliwataka wachimbaji hao kuachana na suala la utoroshaji wa madini na kuyauza kwa njia za magendo huku akionya kwamba, yeyote atakayekamatwa, atawajibika kisheria.

Awali, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali Shaban Lissu, Naibu Waziri alimsisitiza kuhakikisha Ofisi yake inaimarisha ulinzi katika njia zote za panya, ili kudhibiti utoroshwaji wa madini.

Kwa upande wao, wachimbaji wadogo wa Kyerwa, wakiwasilisha maombi yao kwa Serikali, walimwomba Naibu Waziri kupatiwa leseni katika maeneo mbalimbali.

Akijibu maombi hayo, Naibu Waziri aliwaahidi kuwa Leseni zitaanza kutolewa na kuhuishwa mara tu Tume ya Madini itakapoanza kufanya kazi, ambapo alisema anaamini itakuwa ni hivi karibuni.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi