[caption id="attachment_46405" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Juliana Shonza akikimbia leo Agost 31 kuashiria ufunguzi wa mbio za riadha ya Kondoa Irangi Marathon mwaka 2019 zitakazofanyika Jijini Dodoma.[/caption]
Na Shamimu Nyaki –WHUSM DODOMA
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amesema kuwa watanzania wanao wajibu wa kulinda,kuthamini na kuendeleza Utamaduni wa nchi katika shughuli zote za uzalishaji pamoja na za kijamii.
Mhe.Shonza ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa maonyesho ya Utalii wa Utamaduni, mambo kale na bidhaa za asili za hapa nchini yaliyoongozwa na kauli mbiu “Utamaduni mambo kale na bidhaa za asili yetu ni fursa ya kibiashara katika utalii” ambayo yalikuwa na lengo la kutangaza utalii wa utamaduni .
[caption id="attachment_46406" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Juliana Shonza akizungumza leo jijini Dodoma wakati alipofunga maoenyesho ya utalii wa utamaduni,mambo kale na bidhaa za asili za Tanzania yaliyofayika kuanzia Agosti 26 – 31, 2019 yaliyoongozwa na kauli mbiu; “Utamaduni,mambo kale na bidhaa za asili yetu ni fursa ya kibiashara katika utalii” .Kulia ni Mkurugenzi na Mratibu wa YaKwetu Fair Dodoma Bw.Japhet Jackson.[/caption] [caption id="attachment_46407" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi na Mratibu wa YaKwetu Fair Dodoma pamoja na Kondoa Irangi Marathon 2019 Bw.Japhet Jackson akitoa maelezo mafupi kuhusu maoenyesho ya utalii wa utamaduni,mambo kale na bidhaa za asili za Tanzania yaliyofayika kuanzia Agosti 26 – 31, 2019 Jijini Dodoma yaliyoongozwa na kauli mbiu; “Utamaduni,mambo kale na bidhaa za asili yetu ni fursa ya kibiashara katika utalii” ambayo yamefungwa rasmi leo na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Juliana Shonza (kulia) .[/caption]Naibu Waziri Shonza ameeleza kuwa lengo la matamasha ya Utamaduni ni kutangaza utamaduni wa nchi yetu unaojumuisha vitu mbalimbali ikiwemo lugha ya Kiswahili,ngoma za asili,bidhaa za asili chakula pamoja na mila na desturi za jamii zetu.
“Hatuwezi kuwa na Taifa ambalo halienzi Utamaduni wake pamoja na lugha yake ya asili ya Kiswahili ambayo sasa ni lugha ya nne ya mawasaliano katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika (SADC) hivyo watanzania ni lazima tuwe mstari wa mbele katika kuuthamini utamaduni wetu” Mhe.Shonza.
Awali akifungua mashindano ya riadha ya Kondoa Irangi Marathon Mhe.Shonza amesema kuwa michezo inasaidia kuibua vipaji ambapo amewataka wananchi wa Jiji la Dodoma kuwa mstari wa mbele katika kushiriki mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Jijini hapo kwakua ndio wenyeji wa Makao makuu ya nchi hivyo wasiwaachie wageni pekee.
[caption id="attachment_46410" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Juliana Shonza akikagua mabanda ya bidhaa za asili za wajasiriamali wa Tanzania leo jijini Dodoma kabla ya kufunga maoenyesho ya utalii wa utamaduni,mambo kale na bidhaa za asili za Tanzania yaliyofayika kuanzia Agosti 26 – 31, 2019 yaliyoongozwa na kauli mbiu; “Utamaduni,mambo kale na bidhaa za asili yetu ni fursa ya kibiashara katika utalii”.[/caption] [caption id="attachment_46411" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Juliana Shonza akigawa zawadi kwa washindi wa mbio za ufunguzi za Kondoa Irangi Marathon mwaka 2019 zilizofanyika leo Agosti 31 Jijini Dodoma.[/caption]Kwa upande wake Mkurugenzi wa Yakwetu Fair Dodoma Bw.Japhet Jackson ambaye ndio mratibu wa maonyesho hayo amesema kuwa lengo la kufanya maonyesho hayo ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kuutangaza Mkoa wa Dodoma kama Makao Makuu ya nchi pamoja na kutangaza fursa zilizopo ili kuvutia watalii wengi na wawekezaji kufka Jijini hapo.
Bw.Japhet Jackson ameongeza kuwa maonyesho hayo yatakuwa endelevu ambayo yatafayika kila mwaka na yatalenga kutangaza utalii wa utamaduni pamoja na vivutio vya asili vilivyopo mikoa ya kusini ambayo imekuwa haitangazwi vizuri ikiwemo kimondo cha mbozi,mto ruaha,kitulo na mbuga ya Selous.
“Maonyesho haya yanalenga kuwainua wafanyabiashara wa bidhaa za Utalii na Utamaduni ambazo zinatangaza nchi yetu kutokana na upekee wa bidhaa hizo”alisema Bw.Japhet.
Naye mshiriki wa maonesho hayo Bw.Emmanuel John amesema maonyesho hayo yamewapa fursa ya kutangaz bidhaa zao pamoja na kupata nafasi ya kufika Jiji la Dodoma mbalo kwa sasa ndio makao makuu ya Serikali.
Maonyesho hayo yamefanyika kuanzia Agosti 21 na yamehitimishwa leo Agosti 31 ambapo baadhi ya shughuli za kiutamaduni zilifanyika ikiwemo kuonyesha mavazi ya asili,ngoma za asili michezo ya jadi na shuguli nyingine za utamaduni.