[caption id="attachment_50148" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF Bw. Christopher Mapunda (katikati)akiongea na waandishi wa habari kuhusu mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya ambapo aliwaeleza kuwa mpango huu utajumuisha kundi mkubwa la watanzania ambao wapo nje ya mfumo wa Bima ya Afya, Kulia ni Meneja Uhusiano wa NHIF Bi. Angela Mziray na Kushoto ni Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja Bw. Hipoliti Lello.[/caption] [caption id="attachment_50150" align="aligncenter" width="750"] Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa NHIF Bw. Hipoliti Lello akitoa mada kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha kuhusu mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya vilivyozinduliwa hivi karibuni.[/caption]
NA MWANDISHI WETU-ARUSHA
Mfuko wa Taifa wa bima ya leo umekutana na waandishi wa habari mkoani Arusha kwa lengo la kuwaelimisha kuhusiana na vifurushi vipya vya bima ya afya.
Akiongea wakati wa Mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Christopher Mapunda amesema kuwa mpango huo una lengo la kuhakikisha idadi kubwa ya watanzania wanakuwa na Bima ya Afya ili kuwa na uhakika wa matibabu.
“Uanzishaji wa mango huu wa Vifurushi vya Bima ya afya ni fursa kwa wananchi kujiunga na bima ya afya kuanzia kiwango cha 192,000 na kuwawezesha kupata huduma ya uhakika wa bima ya afya.
[caption id="attachment_50149" align="aligncenter" width="750"] Meneja wa NHIF Mkoa wa Arusha Bw. Isaya Shekifu akiongea na waandishi wa habari Mkoa wa Arusha ambapo aliwasihi kuwa mabalozi wazuri wa mpango huu wa vifurushi vya Bima ya Afya.[/caption] [caption id="attachment_50151" align="aligncenter" width="750"] Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha wakifuatilia mada zilizowasishwa na NHIF kuhusu mpango wa vifurushi vya Bima ya Afya.[/caption]Aidha, Bw. Mapunda alisema kuwa NHIF imeendelea kutoa elimu kwa umma wa watanzania kuona umuhimu wa kuwa na Bima ya Afya kwa ajili ya matibabu ya uhakika.
Akiongea kwa niaba ya Waandishi waliohudhuria Mkutano huo Mwenyekit wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha Claud Gwandu alisema kuwa kwa jinsi hali ilivyo sasa ni muhimu kwa kila mwananchi kujiunga na mpango huu wenye nia ya kuwasaidia wananchi wengi zaidi.
[caption id="attachment_50147" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama NHIF Bw. Christopher Mapunda akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa Habari Mkoani Arusha,baada ya kuwapa elimu kuhusu mpango wa vifurushi vya Bima ya Afya.[/caption]“Hatukuwa tunaelewa namna vifurushi hivi vinavyofanya kazi, ila baada ya elimu hii nimeona ndio suluhisho, watanzania waone umuhimu wa kujiunga, kwasasa gharama za matibabu kwa sasa ni kubwa sana ila kwa vifurushi hivi kwa mfano 192,000 inakuwezesha kupata matibabu kwa mwaka mzima”-Alisema Bw. Gwandu
Naye Meneja wa NHIF Mkoa wa Arusha Bw. Isaya Shekifu amewashukuru waandishi waliohuria kikao hicho na amewasihi kuwa mabalozi wazuri wa vifurushi vipya vya bima ya afya.