Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Nanenane 2023, Kuanza Rasmi Leo
Aug 01, 2023
Na Byarugaba Innocent - Morogoro

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Mhandisi Mshamu Ali Munde amefika mkoani Morogoro kushiriki ufunguzi wa Sherehe za Wakulima maarufu kama Nanenane Kanda ya Mashariki.

Tayari Mhandisi Munde amefanya ukaguzi wa awali kwenye mabanda ya Mifugo, Ufugaji wa Samaki na Vipando vya Mazao ya Chakula na Mbogamboga pamoja na bidhaa za usindikaji.

Aidha, Mhandisi Munde kwa ujumla ameridhishwa na maandalizi yote yaliyofanywa yakiratibiwa na Bw. Charles Marwa, Mkuu wa Divisheni ya Mifugo, Kilimo na Uvuvi  wa Halmashauri ya Mji Kibaha.

Bw. Marwa amemweleza Mhandisi Munde kuwa Halmashauri ipo tayari kushiriki na kushindana kwani Wakulima, Wafugaji na Wajasiliamali Wana Ari, shauku na nia ya kushiriki kikamilifu ili kurudi na ushindi.

Kauli mbiu ya sherehe za nanenane mwaka 2023 inasema "Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula" ambapo Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Peter Pinda anatarajiwa kufungua rasmi maonesho hayo leo Agosti 1, 2023 kwenye Kanda ya Mashariki inayoshirikisha Mikoa ya Dar -es-Salaam, Pwani, Morogoro na Tanga.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi