Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Afanya Mazungumzo na Balozi wa China Nchini
Nov 14, 2017
Na
Msemaji Mkuu
<
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba na Balozi wa China nchini Mhe. WANG Ke wakifuarahia jambo walipokutana kwa mazungumzo Wizarani Mjini Dodoma.Naibu Waziri amemuhakikishia Mhe.Balozi WANG Ke kuwa Wizara na Serikali wataendelea kudumisha uhusiano wa kahistoria uliodumu kwa muda mrefu baina ya Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China. Pia Mhe. Dkt. Kolimba alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya China kwa kufadhili miradi mbalimbali hapa nchini.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba na Balozi wa China nchini Mhe. WANG Ke wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo