Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Masauni Akagua Makazi ya Askari Yaliyouzwa Kinyume na Utaratibu
Jan 27, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_27974" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuuliza maswali Mhandisi wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Pascal MacORWA (kushoto), alipotembelea eneo la Tunguu lililovamiwa na wananchi, ambalo mmiliki halali ni jeshi la Polisi. Wa kwanza kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja,Makarani Khamis na watatu kulia ni Mkuu wa mkoa huo, Hassan Khatib Hassan.Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.[/caption] [caption id="attachment_27975" align="aligncenter" width="750"] Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Makarani Khamis , akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, juu ya eneo la Tunguu lililoko Mkoa wa Kusini Unguja ambalo ni mali ya Jeshi la Polisi, hivi sasa likimilikiwa na wananchi kinyume cha sheria.Kushoto ni Mkuu wa mkoa huo, Hassan Khatib Hassan. Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.[/caption] [caption id="attachment_27976" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyeshwa na Mhandisi wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Pascal MacORWA, ramani ya moja ya maeneo yanayomilikiwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa ziara yake ya kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi mkoani hapo.Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo,Hassan Khatib Hassan.[/caption] [caption id="attachment_27977" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatib Hassan, akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kukagua makazi ya askari polisi yanayoonekana pichani, yaliyopo eneo la Machui, lililopo Mkoa wa Kusini Unguja.Naibu Waziri yupo Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi na makazi ya askari.Kulia ni Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoani hapo.[/caption] [caption id="attachment_27978" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatib Hassan, akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kukagua eneo yalipojengwa maduka ya biashara ambayo wamiliki wamenunua viwanja hivyo vya Jeshi la Polisi kinyume na utaratibu. Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.[/caption] [caption id="attachment_27979" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa Mkoa Kusini Unguja alipowasili leo mkoani hapo kwa ziara ya kikazi ya kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi na makazi ya askari.Kulia ni Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi