Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Madini Atembelea Machimbo ya Jasi
Dec 12, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_24689" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akishuhudia upakiaji wa Madini ya Jasi katika kijiji cha Kihanju, Itigi yanayosafirishwa kuelekea kwenye Kiwanda cha Saruji cha Mbeya Cement ikiwa ni moja ya malighafi ya kutengenezea Saruji[/caption]   [caption id="attachment_24690" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akiwasikiliza wachimbaji na wafanyakazi wa machimbo ya Jasi, yaliyopo katika Kijiji cha Kihanju, Itigi, Mkoani Singida alipofanya ziara kwenye machimbo hayo.[/caption] [caption id="attachment_24691" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kushoto) akitazama hatua ya uchomaji wa Madini ya Jasi kwenye kiwanda cha kampuni ya mzawa cha RSR kilichopo katika Kijiji cha Sanjaranda, Itigi kabla ya kusagwa kuwa unga na baadaye kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kuuzwa na mwingine kutumika katika Kiwanda cha kutengenezea mapambo ya Majumbani, katika kiwanda kilichopo Singida mjini.[/caption] [caption id="attachment_24692" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kulia) akikagua mitambo ya kusagia mawe ya Madini ya Jasi kwenye Kiwanda cha kutengeneza Chaki cha Dobercolor kilichopo katika Kijiji cha Majengo, Itigi.[/caption] [caption id="attachment_24693" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akitazama Chaki zinazozalishwa na Kiwanda cha Dobercolor kilichopo katika Kijiji cha Majengo, Itigi ambazo huuzwa ndani na nje ya Mkoa huo huku lengo likiwa ni kuuza nje ya Tanzania.[/caption] [caption id="attachment_24694" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kulia) akimsikiliza Meneja wa kiwanda cha kutengeneza Chaki cha Furaha, kilichopo katika Kata ya Tambukareli, Itigi, Peter Nolasco (kulia) akielezea namna Madini ya Jasi yanavyosagwa na kuwa unga (Gypsum powder) kwa ajili ya kutengenezea Chaki.[/caption]

Na.Mwandishi Wetu, Singida

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amefanya ziara kwenye machimbo ya Jasi (Gypsum) ya Mkoani Singida na kuzungumza na Wafanyabiashara na Wachimbaji wa Madini hayo ambapo aliwahakikishia ushirikiano wa dhati wa kufikia malengo waliyojiwekea.

Alitembelea maeneo ya machimbo ya Madini ya Jasi na Viwanda vidogo vya uongezaji thamani ya madini hayo ikiwemo viwanda vya kusaga madini ya Jasi ambayo unga wake unasafirishwa nje ya Mkoa huo, viwanda vya kutengeneza chaki vilivyopo Itigi na kiwanda cha utengenezaji wa mapambo ya majumbani kilichopo Singida Mjini.

Naibu Waziri Nyongo yupo Mkoani Singida kwenye ziara ya siku Tatu ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uchimbaji wa madini Mkoani humo ili kujionea shughuli zinazofanywa kwenye maeneo hayo na kuzungumza na wachimbaji wa madini ili kubaini changamoto zinazowakabili kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wake.

Kwa mujibu wa wachimbaji wa madini hayo, Madini ya Jasi hutumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kutengenezea chaki, hospitalini kwa watu waliovunjika na kutengeneza viungo bandia, kutumika kutengenezea saruji, urembo majumbani, hutumika kama insulation kwenye majengo makubwa kwa kuwa Jasi huzuia moto, kutengenezea midoli na masanamu, kutengeneza meno bandia na pia hutumika kama mbolea.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi