Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Gekul: Wasanii Zalisheni Kazi Bora Zinazokubalika Kimataifa
Feb 18, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Eleuteri Mangi- WUSM, Dodoma 

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul amekutana na Wasanii wa tamthilia ya Huba na kufanya nao mazungumzo juu ya kuboresha kazi zao ili zikubalike ndani ya nchi na kimataifa.  

Mazungumzo hayo yamefanyika Februari, 18, 2022 katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba jijini Dodoma ambapo Wasanii hao walipata fursa pia kutembelea ujenzi wa jengo jipya la wizara hiyo.

“Asanteni kwa ziara yenu ya kutembelea ofisi zetu hapa Mtumba Mji wa Serikali, kwetu sisi ni heshima na faraja. Huo ni uungwana na upendo, sisi tunauthamini jitihada zenu. Hakika tamthilia yenu ya Huba ni nzuri, watu wanaifuatilia sana”, amesema Mhe. Gekul.

Akiongea na wasanii hao, Naibu Waziri Gekul amesema kuwa wizara hiyo imekuwa sikivu na inaendelea kusimamia sekta zilizo chini yake kwa kuzingatia maelekezo ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambayo kila mara amekuwa akisistiza Serikali inapaswa kuwa karibu na wadau wake.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Bw. Eliya Mjatta amesema tamthilia Huba imekuwa jukwaa la kuitangaza nchi ya Tanzania zaidi ya miaka sita kimataifa kupitia kisimbuzi cha DSTV chaneli ya Maisha Magic Bongo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi