Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Biteko Atamani Madini Yachangie Zaidi Pato la Taifa
Jan 15, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_27113" align="aligncenter" width="982"] Naibu Waziri mpya wa Madini Dotto Biteko (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (kulia), alipowasili Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma leo, Januari 15 2018.[/caption]

Na: Veronica Simba – Dodoma

Naibu Waziri mpya wa Madini, Dotto Biteko ameeleza kuwa anatamani kuiona sekta ya madini ikichangia zaidi ya ilivyo sasa katika Pato la Taifa.

Ameyasema hayo mapema leo, Januari 15 mjini Dodoma, alipowasili rasmi katika Ofisi yake ya Makao Makuu na kupokelewa na viongozi mbalimbali pamoja na watumishi wa Wizara ya Madini na wa Wizara ya Nishati.

Amesema kuwa, sekta ya madini inaweza kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa kutoka asilimia Nne ya sasa na kuweza kufikia asilimia 10 au zaidi ikiwa kutakuwa na ushirikiano baina ya wafanyakazi wote na viongozi wa Wizara huku kila mmoja akijituma kutimiza wajibu wake ipasavyo.

[caption id="attachment_27117" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri mpya wa Madini, Dotto Biteko akisalimiana na watumishi mbalimbali wa Wizara ya Madini, Wizara ya Nishati na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), alipowasili Makao Makuu ya Wizara, Dodoma mapema leo Januari 15, 2018.[/caption]

“Tujiulize hivi ni kwanini hadi leo sekta hii inachangia asilimia Nne tu katika Pato la Taifa badala ya kupanda hadi asilimia 10 au zaidi. Tubainishe ni madini yapi yanayotupatia fedha nyingi zaidi na ni mbinu gani tutumie ili tuweze kupanda zaidi,” amesisitiza.

Hata hivyo, Naibu Waziri Biteko alibainisha kuwa ujio wake wizarani haulengi kubadili au kugeuza mambo bali ni kuongeza nguvu zaidi kwa watangulizi wake katika kutekeleza yale ambayo yameagizwa na Mheshimiwa Rais John Magufuli kwa niaba ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Tuombeane kwa Mungu atupe kibali, hekima na uwezo wa kuyaona matatizo lakini zaidi sana atupe uwezo wa kutekeleza majukumu yetu ili sekta hii ya madini iwe sekta ambayo ina mchango mkubwa kwa Taifa letu.”

[caption id="attachment_27118" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akifurahia jambo na Naibu Waziri mpya wa Madini Dotto Biteko (kushoto kwa Waziri) alipofika ofisini kwake kumsalimu mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara Dodoma. Wengine pichani ni viongozi mbalimbali wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati.[/caption] [caption id="attachment_27119" align="aligncenter" width="750"] Kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziri mpya wa Madini Dotto Biteko na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, wakifurahia jambo ofisini kwa Waziri, wakati wa mapokezi ya Naibu Waziri Biteko Makao Makuu ya Wizara Dodoma.[/caption]

Aidha, amesema kuwa falsafa yake ya utendaji kazi ni kwa kila mmoja kuheshimu nafasi ya mwenzake bila kujali nafasi aliyonayo. “Binafsi ninaamini hakuna mkubwa kwenye kufanya kazi. Ukubwa wako unaonekana kwenye matokeo ya kazi unayofanya. Kwa hiyo tushirikiane wote. Mimi ninaamini katika nguvu ya ushirikiano,” amesisitiza.

Viongozi mbalimbali waliompokea Naibu Waziri Biteko akiwemo Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Katibu Mkuu wa Madini Profesa Simon Msanjila, wamemwahidi ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wote wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati, Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga amempongeza Naibu Waziri kwa kuteuliwa katika nafasi hiyo na kueleza kwamba

[caption id="attachment_27120" align="aligncenter" width="620"] Naibu Waziri mpya wa Madini Dotto Biteko, akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati (hawapo pichani), alipowasili Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Januari 15 mwaka huu.[/caption] [caption id="attachment_27121" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (kushoto) akizungumza, wakati wa hafla fupi ya kumpokea Naibu Waziri mpya wa Madini, Dotto Biteko (katikati) Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Januari 15 mwaka huu. Kulia ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo.[/caption] [caption id="attachment_27122" align="aligncenter" width="675"] Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga akitoa salamu za kumkaribisha Naibu Waziri mpya wa Madini, Dotto Biteko (hayupo pichani) kwa niaba ya wafanyakazi wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati.[/caption] [caption id="attachment_27128" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya wafanyakazi wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati, wakimsikiliza Naibu Waziri mpya wa Madini, Dotto Biteko (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma Januari 15 mwaka huu.[/caption]

wafanyakazi wanayo imani kubwa kuwa atasimamia vema utekelezaji wa majukumu katika sekta husika.

“Hii ni kwa sababu tunaamini unaifahamu vema sekta ya madini kutokana na kuwa umekuwepo kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa muda mrefu na umeweza kuisimamia vizuri.”

Wafanyakazi wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati wana uhusiano wa karibu kikazi kutokana na kufanya kazi kwa pamoja kwa muda mrefu katika iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini kabla ya kutenganishwa na kuwa Wizara mbili tofauti. Hii ndiyo sababu wangali wanashirikiana katika mambo mbalimbali kama hafla hii ya kumpokea Naibu Waziri.

Naibu Waziri Biteko aliteuliwa katika nafasi hiyo Januari 6 mwaka huu na kuapishwa tarehe 8 Januari na Rais John Magufuli.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi