Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Katibu Mkuu Nishati Awasili Ofisini Rasmi
Mar 11, 2024
Naibu Katibu Mkuu Nishati Awasili Ofisini Rasmi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio wakati alipowasili rasmi ofisi za wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma
Na Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio  amewasili rasmi ofisini na kuahidi kumsaidia Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake kwa Taifa.

Alipowasili ofisi za wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma, alipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mha. Felchesmi Mramba, menejimenti na watumishi wengine wa wizara hiyo.

Akizungumza mara baada ya mapokezi, Dkt. Mataragio amesema ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi ni nyenzo muhimu ya kuyafikia matarajio ya viongozi wa kitaifa na Taifa kwa ujumla.

"Mimi  nashukuru kuteuliwa kutumikia nafasi hii, nitaendelea kushirikiana na watumishi wenzangu ili kumsaidia Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake." Amesema Dkt. Mataragio.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi