Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Wawasilishwa kwa Kamati
Aug 30, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge na Uratibu imewasilisha Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.

Kikao hicho kilihusisha viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene na Naibu Waziri wake, Mhe. Ummy Nderiananga. Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. John Jingu pamoja na Naibu wake, Kaspar Mmuya.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi